Jeshi la Polisi Lawatawanya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Dodoma Ambao ni Wafuasi wa Chadema Kwa Kufanya Mahafali Bila Kibali

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma  limewasambaratisha wanafunzi  wa vyuo vikuu  wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO ... thumbnail 1 summary
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma  limewasambaratisha wanafunzi  wa vyuo vikuu  wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO ) waliokuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika  Ukumbi wa African Dreams  ulipo Area D mjini Dodoma.
 
Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi wamekamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao. 

Polisi wamesema mikusanyiko  yote ya kisiasa ilishapigwa marufuku, hivyo hata mahafali hiyo ilikuwa batili