Madai ya Sumu Ofisini Kwa Meya wa jiji la Mwanza yasababisha Kikao Kuvunjika....

Kikao cha kamati ya fedha na uongozi cha halmashauri ya jiji la Mwanza, kimevunjika baada ya Meya wa jiji hilo James Bwire kulalamikia ha... thumbnail 1 summary
Kikao cha kamati ya fedha na uongozi cha halmashauri ya jiji la Mwanza, kimevunjika baada ya Meya wa jiji hilo James Bwire kulalamikia harufu kali, inayohisiwa kuwa ni sumu iliyokuwa ikitoka kwenye kiyoyozi ndani ya ofisi yake, huku watumishi wawili wa jiji hilo wakishikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Adam Mgoyi amethibitisha kusambaratika kwa wajumbe wa kikao hicho.

Watumishi wanaohojiwa na jeshi la polisi ni katibu muhtasi wa ofisi ya mstahiki Meya Gladys Chiduo pamoja na karani wa ofisi hiyo Anselemi Mtobesya.

Mstahiki Meya James Bwire, ambaye mwezi aprili mwaka huu alilazwa katika hospitali moja jijini Nairobi nchini Kenya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kudaiwa kuanguka ghafla ofisini kwake, anaeleza hali aliyoikuta ofisini kwake wakati alipoingia maliwatoni kwa ajili ya kujisaidia wakati kikao hicho kilipokuwa kinaendelea.

Diwani wa kata ya Mbugani Mahamoud Jama pamoja na Hanifa Mhere ambaye ni diwani wa viti maalum wanasimulia kwa kina kuhusiana na tukio hilo ambalo limetokea hii leo baada ya wajumbe wa kamati hiyo kumaliza kutembelea miradi ya jiji iliyopo eneo la Community Centre kata ya Mirongo na Sinai kata ya Mabatini ambako eneo kwa ajili ya machinga limetengwa.